Wednesday , 26 October 2016
Latest News

Mr. Chuz: Jumba la dhahabu sasa linarudi kivingine kabisa.

TAMTHILIA iliyowashika watazamaji kutoka Swahiliwood imerudi katika staili nyingine inayotarajia kuwashika watazamaji kutokana na maandalizi yake ilivyotengenezwa na kuwashirikisha wasanii wa awali na wasanii wapya wenye majina katika tasnia ya filamu, awali kundi ambalo lilikuwa likionyesha mchezo wake katika televisheni ya Taifa yaani TBC 1, ilisimama na kuonyesha tamthilia nyingine ambayo imemalizika na kuanza maandalizi ya Jumba la Dhahabu season 2 inayotarajia kuwateka watazamaji.

Ahmed Olotu

Mzee Chilo mwigizaji wa filamu na tamthilia.

Zubery Mohamed

Wasanii wa Jumba la Dhahabu wakiwa katika picha ya pamoja.

Tuesday Kihangala

Mr. Chuzi akiwa katika pozi.

“Siku zote tunajali maoni ya watazamaji wetu ambayo wanatoa kwetu sisi, wapenzi wengi wameomba tamthilia ya Jumba la Dhahabu iendelee baada ya kuona katika Dvd ambazo ziliingia mtaani kwa ajili ya mauzo, kwa sababu tunaamini kuwa watazamaji siku zote ndio mabosi wetu basi hatuna budi kutekeleza maoni yao na ukweli ni kwamba tunatarajia kuzoa wapenzi wengi zaidi kuliko awali,”anasema Mr. Chuzi.

Tamthilia ya Jumba la Dhahabu inaandaliwa na Tuesday Entertainment Ltd chini ya mkurugenzi Tuseday Kihangala na amesema kuwa moja ya sababu ya Jumba la Dhahabu kujinyakulia umaarufu ilitokana na kuonyeshwa kwa wiki mara tatu lakini kwa sasa igizo hilo litakuwa likirusha mara tano kwa wiki yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, pia wale wasanii wote maarufu waliotamba na kuvuma katika tamthilia hiyo wamerudi wote, akina Mzee Chilo, Bad boy, Jina Kabula, Winta, Mr. Chuzi na wengine wakali wataoneka katika tamthilia hiyo itakayorushwa TBC1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*