CHAMA cha Baiskeli Mkoa wa Lindi (CHABALI), kinaendelea na zoezi lake la kusaka vipaji vya vijana katika vijiji mbalimbali ambao wataundaa timu ya mkoa huo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Lindi jana, Katibu Mkuu wa CHABALI, Said Kengele, alisema kwa njia ya simu akiwa Lindi, kwamba anachokifanya kwa sasa ni kusaka wachezaji na wadhamini.
“Haijalishi kutokuwa na wadhamini, nitaendelea na zoezi la kusaka vijana, kwani wakijitokeza tutakuwa na wachezaji wengi,” alisema.
Alisema bado hajakata tamaa ya kuendelea kusambaza mchezo huo nchini, licha ya kukosa sapoti kutoka kwa wadau mbalimbali.
“Nimekuwa nikienda mikoa mbalimbali kuhamasisha mchezo huu, lakini nimekuwa nikijigharamia mwenyewe, kitendo ambacho kinaniumiza lakini sikati tamaa, nitahakikisha natimiza lengo langu,” alisema katibu huyo.
Chanzo: Tanzania Daima