Notice: Undefined offset: 0 in /hermes/bosweb26c/b2754/nf.mylinkspage/public_html/dullonet.com/sports/wp-includes/capabilities.php on line 1067

Wasanii kibao wajitokeza usaili filamu ya Injinia.

Jaqueline Wolper

Jack Wolper mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

FILAMU ya aina yake ya Injinia inayotarajia kuanza kutengenezwa kutoka Swahiliwood imeingia katika hatua nyingine baada ya usaili wa kwanza kwenda vizuri kwa kuwapata wahusika watakaoshiriki katika filamu hiyo, filamu inayotabiriwa kuwa na mapinduzi makubwa kutokana na maandalizi yake huku suala la taaluma na nafasi kwa wahusika zikizingatiwa.

 

Jaqueline WolperJack Wolper mshiriki wa filamu ya Injinia.

Akiongea na FC mmoja wa Waongozaji wa filamu hapa nchini Leah Richard Mwendamseke ‘Lamata’ amesema kuwa wasanii wengi wamepatikana lakini jambo linalowasumbua hadi sasa ni mhusika mkuu katika filamu hiyo akiigiza kama Injinia mwenye taaluma ya ujenzi wa majumba.

“Napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha wasanii kutoka kokote wenye sifa za Injinia tunayemhitaji katika filamu yetu, na hili tunalifanya kwa sababu moja kuu ni kuhakikisha hadithi ya filamu hii inakwenda kama mwandishi alivyokusudia, kwani kwa kufanya hivyo ujumbe utaifikia jamii,”anasema mwandishi wa muswada wa filamu hiyo Lamatha.

Filamu ya Injinia imetungwa na msanii mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Issa Kipemba ambaye pia anatarajia kuigiza katika filamu hiyo, msanii nyota Jaqueline Wolper ni moja kati ya wasanii walipita katika usaili wa filamu hiyo.
.

Issa KipembaKipemba mtunzi na mshiriki wa filamu ya Injinia.

Mhusika mkuu katika filamu hiyo ni kijana mwenye umri wa kati asiye na muonekano wa kushitua jamii hata ukipishana naye hauna mashaka naye lakini ni mwenye akili na ujuzi wa hali ya juu katika matukio, filamu hiyo inaandaliwa chini ya kampuni inayokuja kwa kasi ya Papa zi ya jijini Dar es Salaam kila siku tembelea FC upate mapinduzi ya filamu ya Injinia.

Chanzo: Filamucentral

About Sports