Tamasha la filamu la Grand Malt (TOFF) kufanyika juni 30 2012
TAMASHA kubwa la filamu la wazi Swahiliwood linatarajiwa kuanza mwezi wa sita tarehe 3o mwaka huu, tamasha hilo linajulikana kwa jina la Grand Malt Tanzania open Film Festival (TOFF) tamasha hilo litafanyika jijini Tanga katika viwanja vya Tangamano na litadumu kwa muda wa siku saba, na kwa kila siku zitaonyeshwa filamu tatu.
.
Akiongea na FC mratibu wa tamasha hilo mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya Jijini Dar es Salaam Bwana Mussa Kisoki anasema kuwa kila kitu kimekamilika kwa ajili ya tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa nne toka kuasisiwa kwake.
.
“Tamasha hili limepokelewa vema kwa Jijini Tanga na kwa mwaka huu kutakuwa na mambo tofauti sana kwani pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu kushiriki kuwepo katika tamasha hilo lakini pia kuna semina zitaendeshwa kwa siku hizo ambazo ni wasanii na wadau wengi kujifunza kuhusu sheria za haki miliki na hakishiriki zitatolewa,”anasema Kisoki.
.
Tamasha hilo kwa upande wa burudani kutakuwa na vikundi vya asili, Tanga Stars na vikundi vya burudani kutka jiji la Tanga, siku ya ufunguzi Bendi Tanzania moto ya taarab kutoka jijini Dar es Salaam itafungua siku ya ufunguzi wa maonyesho haya ya kihistoria na kipekee, mnakaribishwa wadau wa tasnia ya filamu wote
Chanzo: Filamucentral




