Notice: Undefined offset: 0 in /hermes/bosweb26c/b2754/nf.mylinkspage/public_html/dullonet.com/sports/wp-includes/capabilities.php on line 1067

Kipemba kurejea katika sanaa.

MWIGIZAJI na Mchekeshaji wa filamu Swahiliwood Issa Kipemba anarudi katika tasnia ya filamu kwa nguvu baada kukaa muda mrefu bila kurekodi wala kujishughulisha na kazi hiyo.

Kipemba anasema kuwa kwa muda huo alikuwa akifanya utafiti kuhusu filamu na sasa amepata jibu kwa ajili ya kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu hapa Swahiliwood.

“Nilikuwepo sehemu mbalimbali nikitafiti kuhusu suala la filamu na soko lake lipo vipi na kama nataka kuingia katika tasnia hiyo, na sasa nimerudi kwa nguvu zote na kuandika filamu ya kipelelezi inayoitwa Injinia, filamu hiyo itakujulisha kuwa kweli Kipemba alikuwa shule kwa ajili ya mambo ya filamu,”

Msanii huyo aliyewahi kujizolea umaarufu akiwa na kundi la Kaole Sanaa Group alisimama akiwa na shughuli zake pamoja na masomo na sasa yupo katika Kampuni ya Papaz inayojishughulisha na mambo ya utayarishaji na usambazaji wa filamu, filamu ya Kipemba inatarajiwa kuanza kurekodiwa hivi karibuni kwani kila kitu kipo tayari zoezi linalofanyika kwa sasa ni kuchagua wasanii wataoshiriki katika filamu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti

About Sports