Notice: Undefined offset: 0 in /hermes/bosweb26c/b2754/nf.mylinkspage/public_html/dullonet.com/sports/wp-includes/capabilities.php on line 1067

Ray the Greatest awaonya wasanii.

Vincent Kigosi

Ray the Greatest Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu Swahiliwood.

MTAYARISHAJI na Muongozaji wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ amewataka wasanii wenzake kufanya sana kazi na kuepukana na majungu au kulaumiana katika vyombo vya habari jambo ambalo yeye anaona linachelewesha maendeleo katika tasnia ya filamu kwani wasanii wamekuwa wakiripotiwa wakilumbana bila sababu ya msingi. KWA HABARI ZAIDI ENDELEA NDANI….

.

Vincent KigosiRay the Greatest akiwa katika pozi.

“Binafsi sipendi sana kuongelea mambo ya mtu zaidi ya kazi yangu ninayoifanya ya filamu na si maisha ya watu binafsi kwani inawezekana kila mtu ana mapungufu yake kama binadamu, ikiwa wewe ni msanii msanii mwenzako akikosea jaribu kumweleza kabla ya kwenda kuongea na vyombo vya habari,”anasema Ray the Greatest.
.

Vincent KigosiRay the Greatest akiingia katika Hotel ya Slipway hafla ya ZIFF.

Ray anasema kuwa kuna baadhi ya wasanii wanatumia vyombo vya habari vibaya kwa kutoa taarifa zinazochafua tasnia hiyo huku wakisahau kuwa kwa kufanya hivyo ni tatizo, hivyo wote wanachafuka na jamii inaweza kuwadharau na kuharibu hata soko la filamu lenyewe, Ray anasisitiza likitokea jambo waongee na kushauriana kabla ya kukimbilia vyombo vya habari.

Chanzo: Filamucentral

About Sports