Nkwabi msanii wa filamu na tamthilia kutoka Swahiliwood.
MSANII wa filamu katika tasnia ya filamu Swahiliwood Nkwabi Juma Jumapili iliyopita alifanya usaili kwa kuchagua wasanii, watayarishaji, waongozaji wa filamu pamoja na wapiga picha wanaotarajia kushiriki katika filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina la Kiduchu Films filamu hizo zitakuwa zikirushwa kupitia Televisheni ya Clouds Tv.
“Nimekuwa nikifikiria njia ambayo inaweza kutoa fursa kwa wasanii wengine kuingia katika tasnia ya uigizaji lakini nafasi zimekuwa chache kwa kushirikiana na Clouds Tv tumebuni Kiduchu Films kipindi kitakachotoa nafasi kwa wale wasanii wenye ndoto za kuigiza lakini wamekosa nafasi hizo,”anasema Nkwabi.
.
Nkwabi amesema kuwa wasanii waliobahatika kuchaguliwa katika usaili huo watapata mafunzo ya fani walizochaguliwa na kuanza kurekodi na vipindi vitarushwa katika televisheni hiyo, vipindi vya Kiduchu films vinatarajia kuanza mapema hivi karibuni.


