Musa Mateja
MCHEZA sinema kiwango Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) amefyatuka kuwa tangu ameingia kwenye sanaa, kila anapopata gari hutuhumiwa kuwa amehongwa hivyo anadai sasa amechoka kuhongwa magari na wanaume.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, Aunt aliweka wazi kuwa kutokana na watu kuendelea kumtuhumu kwa kila kitu anachomiliki kuwa amehongwa, anakoelekea sasa amechoka madai hayo na anachoomba watu waelewe kwamba kila mali aliyonayo kanunua kwa fedha yake.
“Hakuna kitu kinachoniuma kama ninaposikia mtu anaongelea kitu nilichonunua kwa fedha zangu halafu anasema nimehongwa,” alisema Aunt na kuongeza:
“Zamani nilijitahidi kupuuza maneno, lakini siku zinavyosonga yanakuwa mengi, ni vema watu waelewe kuwa chochote nilichonacho sijahongwa.
“Ukweli ni kwamba nimeshahongwa sana magari kwa kuambiwa na watu na sasa nimechoka kusikia hivyo tena na kama kuna mtu ana uwezo wa kunihonga kila siku, basi awe ananielekeza pa’ kuzichukulia fedha au gari kuliko kunizushia kila kukicha.”
Notice: Undefined offset: 0 in /hermes/bosweb26c/b2754/nf.mylinkspage/public_html/dullonet.com/sports/wp-includes/capabilities.php on line 1067
– March 5, 2012Posted in: Habari na Dondoo za Udaku


Wapotezeee!