Mchezaji Uhuru Selemani wa Simba kulia akichuana na beki wa timu ya Villa Squard ya jijini Dar es salaam katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, timu ya Villa Squard imefanikiwa kuifunga Simba goli 1-0 na kujipatia pointi tatu muhimu katika ligi hiyo. Goli la timu ya Villa Squard limefungwa na mchezaji Nsa Job kwa kichwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu katika viwanja tofauti ni kama ifuatavyo Moro United imefungwa goli 1-0 na timu ya Coastal United, Ruvu Shooting Star na Polisi Dodoma zimetoka sare ya 0-0,
