Monday , 24 October 2016
Latest News

Ndoa ya DC Bety Mkwasa na Charles Boniface Mkwasa yatimiza miaka 25.

 Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na  Januari 18 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa.
Wakulima na wananchi kutoka Bahi ambako Mheshimiwa Betty Mkwasa anafanyia kazi walileta kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti lita zaidi ya 30, Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, bata Mzinga na nafaka za mahindi na mchele kwa maharusi.
   Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dodoma wakiwa na wake zao wakipiga picha na maharusi. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Bahi.
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)

About Yusuph Abdul