order cialis side effects without prescription
Wednesday , 1 July 2015
Latest News

Habari za Mahakamani.

Atupwa jela miaka 30 kwa kumlawiti mwanafunzi.

mahakamani iringa

Na Lucas Raphael, Tabora MAHAKAMA ya Wilaya ya Tabora imehukumu Masudi Nassor (20) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka tisa. Akitoa hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bahati Chitepo alisema kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye ... Read More »

Kesi ya udhalilishaji, Makonda apewa siku saba kujitetea.

makonda-300x171

Na Josephine Mwaiswaga, Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imempa siku saba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kuwasilisha utetezi wake kwenye kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya udhalilishaji dhidi ya baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi.   Kesi hiyo ilifunguliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mgana Msindai na aliyekuwa Mwenyekiti ... Read More »

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara aachiwa kwa dhamana.

johnson-minja (1)

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja ameachiwa kwa dhamana na serikali imeambiwa isisikie maneno ya kuambiwa. Mwenyekiti huyo ambaye alifutiwa dhamana Machi 26, alirejeshwa mahakamani leo ambapo kesi yake ilitajwa, akitokea gereza la Isanga. Kwa mujibu wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali Aprili 9 mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo ... Read More »

IPTL yaikimbia kesi yake dhidi ya maazimio ya Bunge.

mahakama rufaa

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imejiondoa katika kesi ya kikatiba iliyoifungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga utekelezaji wa maazimio nane yaliyopitishwa na Bunge baada ya kushindwa kupinga mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa serikali. Mbali na IPTL kampuni nyingine zilizohusika kupinga maazimio hayo ni Pan Africa Power Solution Ltd (PAP) mmiliki wa IPTL, ... Read More »

Kesi ya viongozi wa Uamsho, upelelezi waendelea.

sheikh_uamsho

KIONGOZI wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Shekhe Farid Hadi Ahmed (45) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi bado wanasota rumande kwa kwa kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika. Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Kaluyenda. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka aliomba tarehe nyingine ya ... Read More »

Atupwa jela miaka 60 kwa kufanya ubakaji Bunda.

mahakama ya mwanzo

Na Ahmed Makongo,Bunda. MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, juzi imemhukumu mwanamume mmoja Festo Domisian (30), mkazi wa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kutumikia kifungo cha miaka 60 jela pamoja na kuchapwa viboko 12, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka wasichana wawili kwa zamu akiwa na kisu na kumjeruhi mmoja wao. Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, ... Read More »

Atupwa jela miaka 30 kwa kusaidia ubakaji.

mahakamani iringa

Na Sifa Lubasi, Mpwapwa. MAMA aliyemsaidia mwanawe kubaka , Regina Kigelulye, ametupwa jela miaka 30 sawa na mtoto wake ambaye alikuwa anakabiliwa na kosa la kubaka, Sagimembe Mroso. Mtoto huyo pamoja na kwenda jela miaka 30 amepewa adhabu ya kuchapwa viboko 12, sita akiingia jela na sita akitoka. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa, Paskal Mayumba mwendesha ... Read More »

Mkurugenzi Ilala afunguliwa mashtaka mengine.

kisutu_300_173

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na wenzake 11, jana walifunguliwa mashitaka mengine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kufuta mwenendo wa kesi ya mauaji iliyokuwa inawakabili dhidi ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 mtaa wa Indira Gandhi na kuua watu 29. Uamuzi wa kufutiwa mashitaka ... Read More »

Kesi ya Katiba kuanza kuunguruma leo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza kesi ya msingi ya kikatiba ya Bunge Maalumu la Katiba. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi la Serikali dhidi ya shauri lililofunguliwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Shauri litakalosikilizwa ni la kuomba tafsiri ya kifungu cha 25 cha Sheria ... Read More »