Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Matukio na udhamini Rukia Mtingwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kuwataka wachezaji kujua afya zao kabla ya mashindano.
“ Hii si lazima, ila tumeona ni nafasi nzuri ya kuwapa nafasi wanariadha kupima afya zao kabla ya mashindano kwa ambao wataona wanataka kufanya hivyo, na hii itafanyika pia kwa wakazi wa Dar es Salaam.”
Mtingwa alisema kuwa zoezi hilo ambalo linafanywa kwa ushirikiano wa Chama cha Tiba ya Michezo (TASMA) na wafanyakazi wa huduma ya kwanza, itatolewa bure.
Katibu wa asasi ya kiraia ya Afya Club, Dk. Deogratius Pissa alisema klabu yake imejipanga kuwafanyia uchunguzi wa kifya wanariadha watakaoshiriki mbio za nusu marathon siku moja kabla ya mashindano hayo. “
Tutakuwa na siku ya kwanza kwa wanariadha wa mbio ndefu, na siku ya mashindano basi itakuwa ni nafasi kwa wananchi ambao watataka kujua afya zao,” alisema.
Michuano hiyo inatarajia kushirikisha wanariadha takribani 400 ambao watashindana katika mbio za nusu marathon na zile za burudani za kilomita tano.
.
Posted by Dullonet: 28.05.2009 Source:
Written by: Mwandishi Maalumu