HALMASHAURI ya wilaya ya Tabora,(Uyui),mkoani Tabora,katika mwaka wa fedha wa 2010/2011,inatarajia kukusanya fedha kiasi cha bilioni 18.2 katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato yake.
Hayo yalisemwa na mweka hazina wa halmashauri hiyo,Angelo Mgongolwa, kwenye kikao cha kawaida cha bajeti kilichoketi kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo wilayani humo.
Mgongolwa alisema kwamba katika fedha hizo,makusanyo hayo yatatokana na mapato ya ndani,fidia ya vyanzo vilivyofutwa(GPG),Wahisani mbalimbali,rzuku ya maendeleo,michango ya nguvu za wananchi na ruzuku ya matumizi ya kawaida.
Alisema katika fedha hizo,halmashauri hiyo iliomba kuidhinishiwakiasi cha sh bilioni 8,046,222,509.00 kwa ajili ya kugharamia matumizi ya kawaida na mishahara ni sh bilioni 8,712,626,330.00 pamoja na nguvu za wananchi sh milioni 165,000,000 ambazo zitatumika kwenye utekelezaji miradi ya maendeleo.
Aidha mweka hazina huyo alisema kwamba katika fedha za ndani kiasi cha bilioni 1,305,751,858.00 zinatarajiwa kutumika kwa matumizi ya kawaida ya kiofisi na utawala.
Aidha alisema katika mapitio ya ya makisio kwa mwaka 2009/10 halmashauri ilikisia kukusanya sh bilioni16,140,301,817.00 ambapo hadi kufikia mwaka 2010 halmashauri ilikusanya sh bilioni 10,128,430,496.08 sawa na asilimia 62.75.
Mweka hazina huyo aliongeza kwamba katika mwaka wa fedha wa 2009/10 halmashauri hiyo ilikisia ilitumia kiasi cha sh bilioni 16,140,301,817.00 hadi kufikia mwezi januari 2010 halmashauri ilikuwa imetumia sh bilioni 6,415,706,837.80 sawa na asilimia 39.75.