Dullonet Tanzania | Korea Kaskazini yajitayarisha kurusha kombora.
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
WAKAZI  wa mji mdogo wa  nansio wilayani  ukerewe mkoani mwanza hawana maji ya bomba kwa zaidi ya siku nne zilizopita  kutokana na sehemu ya kuwashia mitambo ya kusukuma maji kualibika.

Wakuzungumzia tatizo hilo wakazi wa mji huo hasa wamiliki wa nyumba za kulala wageni , migahawa na mahotel wamesema hali ya  usafi katika  vitegauchumi vyao  sio nzuri  hali ambayo  wanaofu  inaweza kusababisha magonjwa  ya mlipuko.

Kwaupande wa  wananchi wa kawaida wanaoitaji maji kwa matumizi ya  nyumbani pia hali inaendelea kuwa mbaya kwasababu  wachuuzi  wanaouza maji wanazidi kupandisha bei  ambapo troli moja  yenye  maji  ya ujazo wa lita 100 iliyokuwa ikiuzwa sh. 300  hivi sasa inauzwa kati y ash 700 hadi 1000 kutegemea na umbali uliopo kati ya ziwani na nyumbani kwa  mteja.

Hali hiyo imewafanya  akinamama na watoto kuacha shughuri nyingine na kuonekana kwa muda mwingi wakitafuta maji  hasa  wakiwa  katika misururu mirefu visimani hali ambayo inapunguza uzalisha mali.

Akizungumzia tatizo hilo afisa wa afya wa wilaya ya ukerewe Bw. Sospeter masanga  amekili kuwa  hali ya usafi katika  hospital ya wilaya hiyo, vituo vya  afya, zahanati na katika nyumba za kulala wageni na mahotel sio nzuri kutokana na tatizo hilo la maji.

Naye meneja wa mamlaka ya maji ya mji wa nansio NAUWASA ,Injinia  Tumaini mugassa amesema tatizo hilo limetokea  baada  ya kifaa kinachotumika kuwashia umeme katika mitambo ya kusukuma maji kuungua  jumapili ya wiki iliyopita.

Hata hivyo amesema tayari ofisi yake imeagiza kifaa hicho kinunuliwe jijini mwanza na kikipatikana kitafungwa  na hali ya uduma ya maji kwa wakazi wa nansio itarejea katika hali ya kawaida na kuwataka wavute subila wakati tatizo hilo likitafutiwa ufumbuzi.




 


Online Radio Live
Posted by Dullonet: 22.04.2010                                                         Source:
Written by: Jovither Kaijage , Ukerewe    


Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.