Dullonet Tanzania | Bodi ya shirika la IAEA lamchagua mkurugenzi mpya
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Posted by Dullonet: 22.04.2010                                                      Source:
Written by:  James Magai
KESI ya madai ya Tume huru ya Uchaguzi(Nne) ambayo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana ilirushwa hadi Juni 8 mwaka huu.

Kesi hiyo namba 84 ya mwaka 2009 ilifunguliwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Samwel Ruhuza, akiwa mlalamikaji wa kwanza na NCCR- Mageuzi akiwa mlalamikaji wa pili, chini ya hati ya dharura (Certificate of urgency) ili iweze kusikilizwa mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Mahakama Kuu ilishindwa kusikilizwa kesi hiyo jana kutokana na serikali kuweka pingamizi ikiiomba mahakama isiisikilize kesi hiyo badala yake iitupilie mbali kwa madai kuwa haina msingi.

Kiongozi wa Jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Njengafibili Mwaikugile aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe hiyo ili kutoa  muda zaidi kwa upande wa mlalamikaji kujibu pingamizi hilo la serikali.

Hata hivyo pande zote zimekubaliana kujibizana kwa njia ya maandishi.

Chama cha NCCR Mageuzi kilifungua kesi hiyo Mahakama Kuu Desemba 17 mwaka jana kikiitaka serikali iunde  Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa madai kuwa Nec ya sasa siyo huru na kwamba kwa muundo wake inatoa nafasi kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kushinda katika uchaguzi mbalimbali.

Katika madai yao, chama hicho kinaitaka serikali kuunda tume huru ya uchaguzi itakayosimamiwa na wadau wote nchini wakiwemo wananchi, viongozi wa dini ili shughuli za uchaguzi nchini zifanyike kwa haki kwa madai kuwa sheria za uchaguzi zilizopo zinakipa nafasi kubwa Chama Cha Mapindunzi(CCM) kuibuka na ushindi.

Pia kinaitaka serikali kuiondoa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na badala yake uchaguzi huo usimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Akizungumzia vifungu mbalimbali vya sheria za uchaguzi ambavyo vinakipa kipaumbele CCM, Mwanasheria wa chama hicho, Raphael Mgaya alisema Tume ya Uchaguzi imeundwa chini ya ibara ya 74 ibara ndogo ya kwanza, ibara ndogo ya 7 inasema tume ya uchaguzi lazima iwe huru, lakini sheria ya uchaguzi inaharibu uhuru wa tume chini ya kifungu cha 4 C na 4D cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985.




















.











Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.