Posted by Dullonet: 22.04.2010 Source:
Written by: Mwandishi Maalum, Morogoro
Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.
Imeainishwa kuwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini MKUKUTA umekabiliwa na changamoto nyingi ambazo hazina budi kufanyiwa kazi katika awamu ya pili ya utekelezaji wa wa mkakati huo.
Changamoto hizo zilizojitokeza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya MKUKUTA I pamoja na usimamizi mbovu wa masuala ya ya fedha , kutoshirikishwa kwa wadau toka asasi za kiraia , miundombinu mibobu ya barabara. Na kutokuwepo utawala bora, na kutokuwepo usimamizi makini kwa vyombo vya sheria.
Hayo yamebainishwa na mktoa mada kutoka wizara ta fedha idara ya kuondoa umaskini bw. Glison timba kwenye mdahalo wa kitaifa kuhusiana maoni na mashauriano ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mkukuta kwa lengo la kuboresha na kufanikisha mkukuta awami ya pili mdahalo uliohusisha wadau kutoka asasi za kiraia za mkoani morogoro
Aidha timba amebainisha kuwa pamoja na changamoto hizo zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa mkukuta awamu ya kwanza yapo mafanikio yaliyojitokeza ikiwemo kupungua kwa vifo vya watoto wachanga kutoka vifo 68 mwaka 2005 hadi kufikia vifo 58 mwaka 2008 kati watoto 100 waluiozaliwa