Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Posted by Dullonet: 21.04.2010
Written by: MILAN, Italia
Kocha wa Inter Milan Jose Mourinho kulia akishangilia na mchezaji wake pamoja na maafisa wa timu hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kuifunga Barcelona magoli 3-1.
FF Inter wameweza kujiweka vizuri katika mashindano ya ubingwa wa ulaya kwa kuwafunga mabingwa watetezi Fc Barcalona kwa magoli 3-1 katika uwanja wa stadio meazza de san siro milano usiku huu na kujiweka kaatika matumaini ya kucheza fainali itakayofanyika Madrid Spain.
Mchezo ulikuwa wa kiufundi haswa kutokana na uchezaji mzuri wa timu ya Barça lakini kwa usiku huu walishindwa kabisa kuukabili mchezo wa nguvu wa timu ya Fc Inter ambao waliweza kuwabana vuzuri uwanjani. Barçalona ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao lililofungwa na mchezaji chipukizi Pedro rodriguez katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza.
Dakika ya 30 kipindi cha kwanza snejder aliweza kuisawazishia timu yake ya Inter,na kipindi cha pili dakika ya 48 maicon aliongeza bao la pili na Diego milito mnamo dakika ya 61 aliweza kuandika goli la tatu ambalo wachezaji wa barçalona walipinga vikali wakidai limefungwa kwa kuotea.mechi ya marudiano itafanyika mjini Barçalona tarehe 28/4 ya mwezi huu
Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.