Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
JOTO la kinyang’anyiro cha ubunge katika Jimbo la Mbozi Mashariki limeanza kufukuta, baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbozi, Aloyce Mdalavuma, kutangaza dhamira ya kugombea jimbo hilo linaloshikiliwa na Mbunge, Godfrey Zambi.
Mbali na mwenyekiti huyo, wanachama watatu akiwamo Zambi kwa nyakati tofauti wametangaza kusaka ubunge katika jimbo hilo linaloonekana kuwa na upinzani wa aina yake kwa wagombea wa CCM.
Wengine waliotangaza dhumuni la kugombea ubunge wa jimbo hilo ni kada maarufu wilayani humo, Jofrey Hasunga.
Mdalavuma ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, alitangaza nia hiyo jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kilichokutana kujadili makadirio ya bajeti.
Alisema ametumia Baraza la Madiwani kutangaza dhamira yake hiyo kwa kile anachoamini kuwa ndipo mahali muafaka kwa kuwa madiwani hao ndio wawakilishi wa wananchi.
Baada ya kumalizika kikao hicho, Mdalavuma alisema nia yake ni kuwasaidia wananchi wa Mbozi Mashariki ambao ni wakulima.
Alisema jimbo hilo lina uchumi mzuri unaotokana na kilimo cha kahawa na mazao ya chakula, lakini cha kushangaza halina mradi wowote wa kitaifa wa maendeleo.
Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
Posted by Dullonet: 21.04.2010 Source:
Written by: Moses Ng'wat, Mbozi
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.