Dullonet Tanzania | Bodi ya shirika la IAEA lamchagua mkurugenzi mpya
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Posted by Dullonet: 21.04.2010                       Source :
Written by:  Mwandishi Maalum
WASHIRIKI wa mashindano ya urembo ya Miss Utalii Tanzania, wametakiwa kutumia nafasi zao katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ili kuhamasisha utalii wa ndani.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na warembo 12 watakaoshiriki shindano la Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini ambalo alitafanyika Aprili 30, kwenye Ukumbi wa Naura Spring Hoteli.

Akyoo alisema fani ya urembo ina nafasi kubwa ya kutangaza utalii hapa nchini, kama warembo watatumia  vizuri nafasi yao  na kutangaza utalii katika jamii.

“Tunawakaribisha sana hapa Ngorongoro muone vivutio vilivyopo na tuna imani mtakuwa mabalozi wazuri wa hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Akyoo.

Katika ziara hiyo, warembo hao walitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kreta ya Ngorongoro, maeneo yenye makundi mbalimbali ya wanyama ndani ya hifadhi hiyo,

Awali Mkurugenzi  wa shindano hilo, linaloandaliwa na kampuni ya Tour Visual Promotion, Anitha  Kajumbula alipongeza NCAA kwa udhamini wao   ambao umewapa nafasi nzuri ya kujua vivutio vya utalii vya Ngorongoro.

Kajumbula alisema siku ya fainali za mashindano hayo yatasindikizwa na bendi ya Ndanda Kosovo iliyohamishia makazi yake mkoani Arusha katika Ukumbi ya Riks.

















.











Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.