Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Posted by Dullonet: 21.04.2010 Source:
Written by: Mwandshi Maalum
MAANDALIZI kwa ajili ya mashindano ya kumsaka Miss Chumbageni, 2010, yameanza huku warembo wakianza kumiminika kwenye Ukumbi wa Tanzanite Club.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Apple Partners Group, ni sehemu ya kuibua warembo wenye vipaji kwa ajili ya shindano la Miss Tanga na baadaye Miss Tanzania.
Mratibu wa mashindano hayo, Suzan Uhinga ilisema kuwa warembo wote wameanza mazoezi japokuwa warembo zaidi wanatakiwa kufika kwa ajili ya shindanmo hilo linalotarajiwa kuwa la aina yake mkoani Tanga.
“Mazoezi yamepangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Tanzanite Club mjini hapa, na warembo wanatakiwa kufika, hii ni nafasi yao kujitokeza katika mashindano waweze kufungua njia za maisha,” alisema Uhinga.
Uhinga alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa wiki mbili na mchujo utafanyika baada wiki mbili kufanyika kwa mashindano hayo.
.
Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.