Dullonet Tanzania | Washiriki tuzo za Kili wapewa somo
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
RAIS wa Shirikisho la Soka TFF, Leodgar Tenga ametangaza azma yake ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria nchini nzima kwa kutumia mpira wa miguu.

Akizungumzia uamuzi wa TFF, rais Tenga alisema amesikitishwa na idadi ya vifo vinavyotokea nchini kila mwaka hivyo anaamini soka ina nafasi kubwa ya kuliokoa taifa kutoka kwenye jenga hili.

"Kwa kila dakika 90 ambazo kunafanyika mechi ya mpira wa miguu hapa nchini watoto 18 hupoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria hii ni takwimu ya kutisha zaidi."

Tenga aliongeza soka ni mchezo wa watu hivyo tunawajibu wa kuungana na serikali pamoja na wadau wote katika kufanikisha kampeni hii ya kitaifa ya kutokemeza ugonjwa huu.

"Tunaamini Watanzania wanapenda soka nadhani itakuwa rahisi kwetu kufikisha ujumbe huu kwa watu wengi kirahisi kwa kutumia mechi mbalimbali zitakazochezwa kwa sasa."

"Kuanzia sasa katika kila mechi ya timu za taifa na zile za ligi tutahakikisha kunakuwa na mabango ya kupinga malaria ili kufikisha ujumbe kirahisi.

"Lengo ni kutaka watu wajue soka ni zaidi ya ligi kuu au Taifa Stars kwani tuna nafasi kubwa ya kutoa mchango kwa jamii wakati wa majanga ili kuwashawishi wazazi kuruhusu watoto kucheza mpira.

Kutokana na athari za ugonjwa huo TFF imeteua mabalozi saba kutoka timu za taifa za soka kwa ajili ya kutangaza kampeni hiyo.

Mabalozi hao ni Kigi Makasi, Juma Jabu, Jonh Bocco na Shaban Nditi kwa upande wa Twiga Stars ni Asha Rashid, Eto Mlezi na Sophia Mwasikile.

Rais Tenga alisema wamechukua uamuzi huo kutokana na athari ya malaria waliyoipata kwa timu ya Taifa Stars walipokwenda nchini Uganda kwenye michuano ya Chalenji.

"Timu ilishindwa kufanya vizuri katika mechi za kwanza kutokana na wachezaji watatu kuugua malaria walipofika Uganda, lilikuwa ni pigo kubwa kwa timu hiyo kutokana na kukosa  mchango wa wachezaji hao," alisema beki huyo wa zamani wa timu ya taifa na Pan Africans.

Naye katibu mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela aliongeza kuwa shirikisho hilo limeanza kampeni hiyo kwa kutoa neti na mafunzo kwa wachezaji 250 wa timu za taifa zote pamoja na vijana walioko kwenye shule ya TFF ya kukuzia vipaji.

"Naamini wachezaji hawa 250 kama kila moja atakwenda kuwaelimisha watu watatu basi ujumbe huu utakuwa umewafikia watu 1000."

Mkufunzi wa Anna McCartney-Melstad alisema hadi mwishoni mwa mwaka huu kila nyumba Tanzania itakuwa imepewa vyandarua viwili hadi vitatu vya bure.
 
Takwimu zinaonyesha zaidi ya watu 80,000 ufa kila mwaka  kwa malaria na wagonjwa milioni 10 hufikishwa hospitali kutokana na Malaria.





Posted by Dullonet: 21.04.2010                                                               Source:
Written by:Mwandishi Maalum



Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
Video za habari na matukio Mbalimbali.
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.