Dullonet Tanzania | Kaseja aingia katika orodha ya makipa wafungaji duniani
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
UZINDUZI wa Filamu ya Lovely Gamble ambayo inamshirikisha muigizaji maarufu nchini Steven Kanumba pamoja na watanzania wanaoishi Uingereza utafanyika Aprili 28 kwenye ukumbi wa Club Billacanas jijini Dar es Salam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET), ambayo imetengeneza filamu hiyo, Asha Baraka, alisema jana kuwa kwa sasa wapo katika maandalizi ya mwisho ili kukamilisha zoezi hilo.

Asha alisema kuwa uzinduzi huo utasindikizwa na burudani ya muziki ya bendi ya Twanga Pepeta na wasanii wengine ambao watangazwa hapo baadaye.

Alisema kuwa hii ni filamu ya pili kwa ASET kutengeneza, kwani mwaka jana walitoa filamu ijulikanayo kwa jina la Tone la Damu ambayo nayo ni moto wa kuotea mbali.

"Hii ni filamu ambayo inazungumzia maisha ya mtanzania Kanumba aliyekwenda Uingereza kwa ajili ya kuwekeza, baada ya kufika kule akanunua hisa kwenye Kampuni ya uzalishaji, lakini hakuweza kufika mbali baada ya kuchanganya kazi na mapenzi," alisema Asha.

Alisema kuwa filamu hiyo itauzwa siku hiyo hiyo ya uzinduzi kwa bei ya kawaida kabisa  ili kuwawezesha wapenzi wa fani hiyo kununua.

Alifafanua kuwa filamu hiyo ina ubora wa hali ya juu kwani hata waigizaji wake ni Watanzania na wa mataifa mengine na asilimia kubwa wametumia lugha ya Kiswahili.

"Mei 29 tutaizundua kwa mara nyingine tena nchini Uingereza ili kutoa nafasi ya uzinduzi kote Tanzania na Uingereza, ni filamu ya kusisimu ambayo kwa kweli imetengenezwa kwa kiwango cha juu," alisema.



.
Online Radio Live
Posted by Dullonet: 21.04.2010                                 Source:
Source:  Mwandishi Maalum


Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........