Dullonet Tanzania | Bodi ya shirika la IAEA lamchagua mkurugenzi mpya
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2010 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Posted by Dullonet: 15.04.2010                                                Source:
Written by:Mwandishi Maalum

Utaratibu wa uchangiaji fedha kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ulizinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Mh.Jakaya Mrisho Kikwete umepokelewa vizuri na wananchi hivyo kuleta matarajio mazuri ya kufikia malengo yaliyowekwa.

Hayo yamebainika katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo ya mako makuu ya CCM jijini Dar Es Salaam.

Richard Hiza Tambwe naibu mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama hicho ameelezea mikakati walioikamilisha katika kinyanganyiro cha uchaguzi kuwa ni pamoja na kununua magari mapya yatakayosaidia wakati wa kampeni pamoja na kujiweka karibu na umma wa watanzania.

Ameongeza kuwa kamati za kufanikisha ushindi zimeshaundwa katika kikao kilichopita cha NEC kilichofanyika jijini Dar Es Salaam na kwamba wanatarajia kupata ushindi mkubwa zaidi wa kishindo kuliko ule wa mwaka 2005.

Hata hivyo Bw. Tambwe ametumia nafasi hiyo kuviomba vyombo vya habari kuendelea kutoa fursa sawa kwa vyama vyote na kutojishirikisha katika utoaji wa taarifa zisizo na ukweli ambazo zinaweza kuleta machafuko katika nchi bila sababu zozote za msingi.

Hivi karibuni kulianzishwa kampeni kwa ajili ya uchangiaji wa fedha za uchaguzi mkuu ambapo CCM ilikamilisha kujipanga kwa ajili ya uchaguzi huo hali ambayo iliwahahakikishia wana CCM kuendelea kufanya vizuri katika uchaguzi ujao





















.











Dullonet Tanzania Online Instant Chatroom
Dullonet Tanzania Online Music
.............Tanzania Website Network...........
Video za habari na matukio Mbalimbali.