Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
MFANYAKAZI wa Benki ya Barclays Ltd, Julius Mpogolo (29), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kujaribu kuiba sh bilioni mbili mali ya benki hiyo.
Wakili wa serikali, Epafras Njau, alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba, kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kisha kuiba fedha hizo.
Alidai, mshtakiwa huyo na wengine ambao hawapo mahakamani kati ya Juni mosi na 3, mwaka huu, katika maeneo yasiyofahamika jijini, walikula njama na kuidanganya benki hiyo kwa lengo la kuiba fedha hizo kutoka akaunti namba 0539200011.
.
.
.
.
.
Posted by Dullonet: 03.07.2009 Source:
Written by: Mwandishi Maalum
Hata hivyo, alidai Juni 3, mwaka huu, mshtakiwa huyo na wenzake waliiba sh milioni 30 kwa kutumia akaunti 001116202 baada ya ya kuhamisha isivyo halali kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye akaunti Na. 0539200011.
Mshtakiwa alikana tuhuma hizo na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika na kutoa fedha au hati ya mali yenye thamani ya sh milioni 15. Kesi itatajwa Julai 17 kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.
.
.
.
.
.