Dullonet Tanzania | Askari Polisi wa Kenya auawa katika tukio la uporaji ng'ombe
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Vikosi viwili tofauti vya doria vya kudhibiti uvuvi haramu mkoani Rukwa vimefanikiwa kukamatwa na kuzichoma moto nyavu haramu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 262 katika kipindi cha mwezi mmoja hadi sasa.

Nyavu hizo haramu zimekamatwa katika msako uliofanywa na kikosi cha  doria cha Kipili wilayani Nkasi na Kasanga wilayani Sumbawanga ambapo nyavu aina ya makokoro na katuli zimekamatwa kwa uwingi.

Akizunngumzia msako huo Kaimu Afisa Mfawidhi wa kikosi cha doria cha Kipili wilayani Nkasi Bw. Cathiberth Raphael amesema kukamatwa kwa nyavu hizo kunafuatia doria za mchana na usiku zilizoendeshwa na kikosi hicho katika eneo lote la mwambao mwa ziwa Tanganyika wilayani Nkasi.


















 





























 





 




 





 
.














.








.













Online Radio Live
Posted by Dullonet: 03.07.2009
Written by: Sammy Kisika, Sumbawanga

Bw. Raphael amesema kikosi chake kimefanikiwa kukamata nyavu zenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 115 na kuongeza kuwa tayari wavuvi wawili wamekamtwa na kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha doria cha Kasanga Bw. Backari Lulela amesema katika kipindi hicho nyavu haramu zenye thamani ya zaidi shilingi Milioni 147 zimekamatwa na kuchomwa moto katika msako ulioendeshwa katika ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga ,ambapo hakuna mvuvi yeyote aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Bw. Lulela amesema kuwa kikosi chake kimekuwa kikifanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa uvuvi wa Sumbawanga na Askari wanyama pori wa wilaya ya Mpanda ambapo katika ziwa Rukwa msako hufanyika kuzunguka ziwa lote hadi katika upande wa wilaya ya Chunya ambako ziwa hilo pia limefika.

Amesema kuendeshwa kwa misako hiyo kumeanza kuleta mafanikio kutokana na wavuvi waungwana kuendelea kuvua samaki wanaokidhi kiwango ihali samaki wakianza kuongezeka na kupatikana kwa wingi.

 


















 














 





























 





 




 





 
.














.








.