Dullonet Tanzania | JKT wakanusha taarifa za kupora ardhi Chita
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Website Designing
We're specialized in developing website's that work. .. More
PC Networking
The Networking  specialises in IT and Network Support ... More
PC Maintenance
PC Repair and Computer maintenance, for the home / business user... More
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
Waziri Mkuu alikuwa akijibu jana swali la msingi la Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF) ambaye alihoji kitendo cha serikali kuigeuka Ilani ya CCM ambayo ilitamka wazi kuwa itaanzisha Mahakama hiyo, huku Mufti akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Katika msisitizo wake, Pinda alisema maelezo ya serikali kuhusu suala hilo ni sahihi ingawa hayatawapendeza wengi, lakini kutokana na Tanzania kuwa na mjumuiko wa dini, imebidi serikali itoe msimamo huo ili kuondoa mitafaruku isiyo ya lazima. Alisema baada ya uchambuzi na umakini uliofanywa, serikali iliamua kuanzisha mfumo mpya wa sheria wa kukidhi haja ya Waislamu, utakaoingizwa katika sheria za nchi katika mwaka huu wa fedha wa 2009/10.

“Katika masuala yanayohusu dini, serikali haina budi kuwa makini katika kutoa uamuzi wake na ndiyo maana tumeamua kuwa na mfumo wa kisheria ambao hauwezi kuleta hisia yoyote mbaya, najua mnaweza msifurahie, lakini nchi kama hii, hatuwezi kutoa uamuzi ambao unaweza kusababisha mtafaruku baadaye,” alisema.

Katika kuongezea uzito wa msimamo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Simba, aliwaagiza mashehe wote wa wilaya, mikoa na wengine Tanzania Bara na maimamu wote nchini kutoa kauli za kupinga uamuzi huo wa serikali. Akizungumza kwa niaba ya Waislamu mbele ya waandishi wa habari na mashehe katika ofisi za makao makuu ya Bakwata, Mufti aliitaka serikali ifute kauli yake na kama kuna utafiti uendelee lakini wa kuangalia kuundwa kwa mahakama hiyo.

Alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, kuwaita mashehe na kupokea maoni yao na kupinga kauli ya waziri huyo kuwa alikutana na wataalamu, ambapo alisema Waislamu hawana uhakika kama alikutana na wataalamu wa dini ya Kiislamu au wengine.

“Waziri (Chikawe) kwa niaba ya serikali amedhihirisha kuwa amewapaka Waislamu mafuta kwa mgongo wa chupa, serikali haijatutendea haki Waislamu imeonesha nchi hii ina wenyewe na Waislamu ni tabaka la pili…haki hii (kuanzisha Mahakama ya Kadhi) tumeidai kwa miaka 20 iliyopita na tumekuwa wavumilivu, sasa tumechoshwa haki zetu kupotoshwa.

“Rais akatutaka Waislamu tutulie na kuahidi kutuletea kitu kizuri, leo limetolewa tamko lisilowafurahisha Waislamu, tunamwomba Waziri afikirie upya suala hili na asilipotoshe ili Rais aonekane amewapotosha au aliwahadaa Waislamu alivyowaahidi, Waziri awape haki zao Waislamu na kuundwa kwa tume kama alivyosema ni kinyume cha haki za binadamu na za Waislamu,” alisema Mufti huku mashehe wakiitikia ‘Takbir’.

Mufti huyo ambaye alitoa tamko hilo kwa takriban dakika 15 na bila kuruhusu maswali ya waandishi wa habari, alihoji iweje Wakristo wakatae mahakama hiyo wakati haiwahusu na kusisitiza: “Pia walitaka misamaha ya kodi irejeshwe na serikali ikawasikiliza, au kwa sababu walisema watawanyima kura?”.

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Waislamu nchini, alisema sheria za Kiislamu haziwezi kuchanganywa na sheria nyingine au kusimamiwa na Wakristo ambao hawana elimu ya sheria za Kiislamu na kusisitiza kuwa kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa Waislamu.

“Waziri anawataka Watanzania wachukulie mfano wa Afrika Kusini na tufuate huko, wakati sisi Waislamu hatujashirikishwa kutoa fikra zetu, tunajuaje kama Waislamu wa huko pia walikubali mfumo huo au la? Kwa nini asichukue mfano wa Uganda, Zanzibar na Kenya, wenye mahakama hiyo? Tunataka mahakama hiyo iwepo kama zilivyo za Ardhi na Kazi”, alisema.

Kuhusu hilo la Afrika Kusini, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania wamwachie Waziri wa Katiba na Sheria awaoneshe namna ambavyo mfumo uliotambulishwa unavyotekelezwa bila kuudhi madhehebu mengine katika nchi ambazo zimefanyiwa utafiti ikiwamo Afrika Kusini. Katika swali la nyongeza bungeni, Mbunge Hemed alitaka kujua kama Ilani ya CCM ilidanganya Watanzania kwa ajili ya kura katika uchaguzi 2005, Spika Samuel Sitta, aliingilia kati na kutetea hoja hiyo akisema:

“Ilani haikusema kama itaanzishwa Mahakama ya Kadhi na si kweli kwamba iliandikwa ili kuvutia wapiga kura, Ilani inasema wazi kabisa kuhusu suala hilo kuwa itashughulikia na kutazama uwezekano wa kuanzisha mahakama hiyo, usiiwekee maneno,” alisema Spika na kufunga mjadala huo.

Hata hivyo, Mufti Simba aliwatoa wasiwasi wananchi kwa kusema kuwa mahakama hiyo haitashughulikia kesi za jinai kwa watu kukatwa mikono, bali kesi za mirathi na ndoa kwa Waislamu pekee. Alisema serikali pia ilishawahi kuahidi kuanzishwa kwa Wakfu, lakini hadi sasa haujaanzishwa wakati kuna Waislamu wasiokuwa na warithi wanaendelea kufariki dunia na mali zao kukosa warithi.

Tamko hilo lilikuja baada ya kauli ya serikali iliyotolewa na Waziri Chikawe wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2009/10 ambapo alisema badala ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, serikali itaingiza misingi ya dini ya Kiislamu katika mfumo wa sheria za nchi.

Alisema viongozi wa dini watakubaliana kuhusu misingi ya dini ya Kiislamu na Waziri huyo atatoa tamko litakalokuwa sheria itakayotambuliwa na mahakama zote nchini. Baada ya Mufti kutoa tamko la Waislamu, mashehe mbalimbali waliokuwa katika ukumbi huo wa Bakwata, waliibuka na kutoa maoni yao wakiunga mkono tamko hilo na kusema wamevumilia vya kutosha, sasa wanataka haki zao ambazo ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.

Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Salum Alhadi, alisema: “Haitawezekana kuchanganya sheria za nchi na za Kiislamu, kwani kwa kufanya hivyo, sheria za Kiislamu hazitafuatwa, hivi ni sawa kusema Imamu wa Msikiti awe John!,” sheria ya Kiislamu haiwezi kusimamiwa na Mkristo”.

Naye Katibu wa Bakwata wa Wilaya ya Ilala, Issa Ausi, aliyeanza kusimama na kutoa maoni mara baada ya Mufti kumaliza, huku akiwa na jazba alisema: “Tumevumilia muda mrefu tumechoka, Mahakama ya Kadhi ilikuwapo, lakini wao wakaiondoa kwa mgambo nyuma, Uhuru wa nchi hii uliletwa na Waislamu, Wakristo walikuwa wapi?”. Naye Shehe Salum Rwambo aliwataka Waislamu kutowapigia kura wabunge na kuwaombea dua wakati wa uchaguzi, kwani wameshindwa kutetea kuwapo kwa mahakama hiyo.