Dullonet Tanzania | Ratiba ya mgawo wa umeme yatolewa.
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Website Designing
We're specialized in developing website's that work. .. More
PC Networking
The Networking  specialises in IT and Network Support ... More
PC Maintenance
PC Repair and Computer maintenance, for the home / business user... More
Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limefanikiwa kuyakamata magari hayo mawili, katika msako uliofanywa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wamiliki.

Kamanda wa Polisi wa mkoa, Lucas Ngíhoboko, akithibitisha matukio hayo, alisema yalitokea juzi saa 3:00 usiku, katika eneo la Shant Town mjini Moshi.

Alisema katika tukio la kwanza, Padre Balige aliporwa gari aina ya Toyota RAV4, baada ya majambazi kufunga barabara kwa mawe na kumshusha na hatimaye kuondoka na gari hilo, lenye namba za usajili T 787 AXD.

Gari hilo lilipatikana baada ya Polisi kuwafukuza hadi kwenye msitu wa Kilelepori huku majambazi hayo yakitokomea.

Kamanda Ngíhoboko alisema katika tukio la pili, juzi alfajiri, majambazi yalipora gari la Francis Mallya (37), lililokuwa limeegeshwa nyumbani kwake, mtaa wa Shaurimoyo mjini Moshi.

Polisi walifanikiwa kulinasa gari hilo likiwa limetelekezwa eneo la Msaranga, huku likiwa limeibwa matairi, taa, redio na vifaa vingine.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna wanaoshikiliwa kutokana na matukio hayo. Polisi bado wanaendelea kuyasaka majambazi hayo.




Online Radio Live