Dullonet Tanzania | Polisi yaamua kuongeza nguvu Tarime
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Website Designing
We're specialized in developing website's that work. .. More
PC Networking
The Networking  specialises in IT and Network Support ... More
PC Maintenance
PC Repair and Computer maintenance, for the home / business user... More
WAKATI majumuisho ya mjadala wa bajeti ya Wizara ya Miundombinu yakiahirishwa hadi leo ili kufanya "marekebisho makubwa", mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), Hundi Chaudhary amesema serikali imeshindwa kutimiza wajibu wake kwenye mkataba wake na Rites wa kuendesha shirika hilo.

Mkurugenzi huyo amesema kampuni yake iko tayari kulirejesha shirika hilo kwa serikali wakati wowote iwapo taratibu za kuvunja mkataba zitafuatwa, ikiwa ni pamoja na serikali kuwekeza fedha zinazolingana na asilimia 49 inazoshikilia kwenye hisa za kampuni hiyo kama mkataba unavyotaka.

.












Posted by Dullonet: 03.07.2009                                                                                                 Source:
Written by: Mwandishi Wetu

Online Radio Live
Mbia mwingine ni kampuni ya Rail India Technical and Economic Services (Rites) inayomiliki asilimia 51.

Akizungumza  jana ofisini kwake, mkurugenzi huyo alisema mkataba huo unaweza kuvunjwa endapo serikali itafuata taratibu na kanuni za kuuvunja.

Sikatai kuuvunja mkataba wala hakuna sababu ya bunge kupiga kelele juu ya mkataba wetu, isipokuwa serikali ikiamua kuuvunja mimi sina pingamizi. Cha msingi wafuate taratibu na kanuni za kuvunja mkataba, alisema Chaudhary akizungumzia hoja za wabunge wengi kuhusu uwezo mdogo wa Rites kuendesha shirika hilo kubwa kwa usafiri unaounganisha mikoa ya kati, Kanda ya Ziwa na Dar es salaam.

Kwanza serikali inapaswa kutoa notisi ya miezi mitatu ikifuatiwa na malipo ya Sh 54.37 bilioni kama fidia ya matumizi mbalimbali ya kampuni hiyo, ikiwepo kuwalipa walinzi wa kampuni ya Ultimate Security inayodai Sh 56 milioni.

TRL imekuwa ikishindwa kuendesha shirika hilo kwa ufanisi, huku ikikabiliwa na matatizo mengi ya wafanyakazi na hasa mishahara ambayo serikali imekuwa ikilazimika kuingilia kati na kulipa.

Mara ya kwanza mwaka jana, serikali ililipa kiasi cha Sh3.6 bilioni ili zisaidie kulipa wafanyakazi wa TRL mishahara ya kiwango cha Sh160,000 kwa kima cha chini kama mkataba na wafanyakazi unavyotaka na mwezi Mei mwaka huu serikali iliamua tena kutoa Sh522 milioni kwa ajili ya mishahara hiyo.

Mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete aliizuia kampuni hiyo kuchukua mkopo ilioomba kwa benki za kimataifa baada ya kubainika kuwa haikuishirikisha serikali katika kufikia uamuzi huo.

Lakini mkurugenzi huyo alisema jana kuwa serikali bado haijalipa kiasi cha fedha kilichotakiwa kuwekezwa kama mtaji wakati wa kuingia mkataba wa kuendesha TRL na kampuni ya Rites. Serikali inamiliki asilimia 49 za hisa za TRL wakati Rites inamiliki asilimia 51.

Akizungumzia suala hilo la fedha za mtaji, Chaudhary alisema: "Sisi hatuna tatizo na wala hatujashindwa kuendesha kampuni hii, isipokuwa suala lililopo hapa ni fedha za uendeshaji.

"TRL inaendeshwa kwa hisa za upande mmoja wa mwekezaji wakati kuna wawekezaji wawili. Mwekezaji wa kwanza ni Rites yenye hisa asilimia 51 na wa pili ni serikali yenye hisa asilimia 49.

Tangu mkataba huu ulipoanza mwaka 2007 mpaka hivi sasa, kampuni inaendeshwa kwa fedha za Rites pekee na ndiyo sababu wananchi na baadhi ya wabunge hawaoni maendeleo yaliyopatikana mpaka sasa.

Mkurugenzi huyo raia wa India alisema wakati wanaanza uendeshaji wa TRL waliikuta kampuni hiyo ikiwa katika hali mbaya huku baadhi ya huduma zikiwa zimesitishwa.

Wakati tunaanza kazi hapa hapakuwa na treni ya kwenda Tanga wala Kigoma... pili treni ya abiria ilikuwa inaishia Dodoma badala ya Dar es Salaam, alisema.

Pia Chaudhary aliongeza kuwa kwa kutumia fedha zake, Rites iliagiza injini 25 aina ya Class 73 za kukodi kutoka India pamoja na na mabehewa 23 ili kuboresha suala la usafirishaji wa abiria na mizigo nchini.

Kampuni hii haikuwa na injini za kutosha na zilizokuwepo hazikuwa na hali nzuri... pia hapakuwa na mabehewa ya kutosha kwa upande wa treni ya abiria.

Serikali imekuwa ikijitetea kuwa inatoa fedha hizo kwa kuelewa kuwa Rites haina uwezo wa kumudu kulipa wafanyakazi mishahara ya kiwango cha sasa, ambacho kilikubaliwa katika mkataba wa hali bora baina ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) na menejimenti ya TRL.

Alisema kabla ya kuhoji utendaji na maendeleo ya TRL, wabunge wanatakiwa kuihoji serikali kuhusu fedha inazotakiwa kuwekeza ambazo ni sawa na asilimia 49 ya hisa zake TRL na kushauri kwamba serikali iwaelimishe wananchi kuhusu mkataba huo.

Serikali haijatoa elimu ya kutosha juu ya mkataba wetu ndiyo sababu ya wananchi kutulaumu kuwa tumeshindwa ingawa ukweli kuhusu hali ya kampuni hiyo kabla ya kubinafsishwa utaendelea kubaki palepale kwa sababu ilikuwa na hali mbaya kuliko ilivyo hivi sasa, aliongeza Mkurugenzi huyo.

Alisema hata suala la kulipa mishahara ya wafanyakazi lilitokana na Rites kuagiza kuwa TRL isilipe mishahara hadi hapo serikali itakapoweka fedha zake kwenye kampuni hiyo.

Nafahamu kwamba wengine wanahoji kuhusu mali zilizopo ila ukweli ni kwamba bila hizo asilimia 51 za Rites, reli hii isingefika hapa ilipofikia.