Dullonet Tanzania | Dar yatikisa kikapukatika michuano ya Majiji
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Entertainment News
Website Designing
We're specialized in developing website's that work. .. More
PC Networking
The Networking  specialises in IT and Network Support ... More
PC Maintenance
PC Repair and Computer maintenance, for the home / business user... More
KOCHA msaidizi wa timu ya vijana, Sylvester Marsh amekisifu kiwango kinachoonyeshwa na vijana wanaoshiriki mashindano ya chini ya miaka 17, Copa Coca Cola na kusema mashindano ya mwaka huu yataipatia Tanzania wachezaji wazuri kwa michuano ya kimataifa.

Akizungumza  jijini jana, Marsh alisema mashindano ya mwaka huu yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na viwango vilionyshwa mwaka huu kupitia kwa wachezaji hawa.

''Inaelekea timu za mwaka huu ziliwaandaa mapema washiriki wa mwaka huu hasa na hii inakuwa rahisi hata kwa makocha kuweza kuchagua vijana bora.



























.






.





.



.







Posted by Dullonet: 02.07.2009
Source: Mwandishi Maalum
Online Radio Live
''Ushindani umekuwa mkubwa kila kijana anaonekana kuwa mzuri zaidi ya mwengine na hii inafurahisha na kilichobaki ni kuwaunga mkono vijana wetu kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwatia moyo wa kufanya vizuri zaidi ya hapo.''

Hata hivyo, katika uteuzi wa timu ya vijana ambayo itaenda kushiriki michuano ya Cecafa (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) nchini Sudan, kati ya vijana watakaofanya vizuri kwenye mashindano haya watachaguliwa kwenye kikosi hicho.

Wakati huohuo TIMU ya soka ya vijana ya Mkoa wa Morogoro jana iliibuka kifua mbele kwa kuishinda Tanga kwa mabao 3-0 yote yakiwa yametinga wavuni kipindi cha kwanza.

Mchezaji Hamis Maulid alifunga magoli mawili, la kwanza likiwa la mapema, dakika ya 3 ya mchezo baada ya kupiga shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Tanga, Idd Hassan.

Bao la pili kwa Morogoro lilijazwa kimiani na mshambuliaji Maulid aliyepiga faulo ndefu ambayo ilizaa matunda katika dakika ya 17 baada ya mchezaji Kulwa Salanga kuchezewa madhambi.

Bao la tatu kwa Morogoro lilifungwa dakika ya 32 kwa pasi ndefu ya Kulwa Salanga iliyomkuta Ally Mnasi na kumalizia.

Michezo mingine inayoendelea leo katika viwanja vinne katika Kundi A, Ruvuma itapambana na Shinyanga ambapo jioni Pwani itacheza na Kilimanjaro, michezo itakayochezwa katika Uwanja cha Karume.

Kutoka Kundi B, kiwanja cha Kawe, Kigoma itaingia uwanjani dhidi ya Pemba Kaskazini na jioni kutachezwa mechi baina ya Rukwa na Mjini Magharibi na katika Kundi C, Mwanza na Tabora watacheza katika kiwanja cha Kawe, huku Kundi D, zitachezwa mechi baina ya Mtwara na Tanga.























.






.





.



.