Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage, alisema klabu hizo ziliwasilisha majina ya wachezaji hao katika muda muafaka ambapo jana ulikuwa mwisho wa kuwasilisha majina hayo.
Kaijage alisema mbali ya klabu za hizo, klabu zingine za Azam FC, Mtibwa Sugar, African Lyon, Moro United, JKT Ruvu, Kagera Sugar na Toto African nazo zimefanikiwa kuwahamisha wachezaji inaowataka kwa ajili ya msimu ujao.
Alisema Azam imefanya uhamisho wa wachezaji watatu, Mtibwa (watano), Afican Lyon (wanne), Moro United (watatu), KT Ruvu na Kagera Sugar kila moja mchezaji mmoja na Moro United 15.
Alisema klabu za Prisons ya Mbeya, Maji maji ya Songea na Manyema FC zimeshindwa kuwasilisha majina ya wachezaji wake hatua inayoonyesha kwamba hazina wachezaji wa kuwahamisha.
Wachezaji wa ndani wa Yanga ni Nelson Kimati (Prisons), Bakari Mbegu (Sifa Politan) na wa kigeni ni Moses Odhiambo (APR), Mwangi Njoroge na Joseph Shikokoti (Tusker), Steven Bengo kutoka SC Villa ya Uganda na Jama Mba Robert kutoka Canon Sportif Yound ya Cameroon.
Kwa upande wa Simba ni Salim Aziz (Polisi Dodoma), Amri Kiemba, Ramadhan Shamte, Juma Kaseja (Huru), Uhuru Seleman (Mtibwa Sugar). Wachezaji wa kigeni ni Dan Mrwanda kutoka Al Tadhamoon ya Kuwait, Joseph Owino kutoka Kenya aliyekuwa akiichezea URA ya Uganda, Hilary Echesa kutoka Uganda (Huru), na Emmanuel Okwi wa SC Villa ya Uganda.
Azam Aggrey Morice kutoka Mafunzo ya Zanzibar, Salum Swedi wa Mtibwa Sugar na Ndayishimiye Christopher kutoka Flamingo ya Burundi. African Lyon, Rashid Gumbo (Mtibwa Sugar), Castory Mumbala (Yanga) Robert Ssentongo kutoka SC Villa ya Uganda na John Mbugua wa Thika United ya Kenya.
Moro United Mahsen Salim (Arusha Stars), Rajabu Mtanda (Korosho SC) na Abubakar Mtiro (Yanga). JKT Ruvu, Kisimba Lumbano wa African Lyon na Kagera Sugar imemuhamisha Diplomate Mustafa kutoka Victor Club ya Uganda.
Toto African imewahamisha wachezaji Laurent Edward, Chesidyo Mathew (Villa Squad), Aman George, Hussein Mataka, Juma Abdi, Athuman Kibarati, Laban Kambole, Jacob Masawe, Moses Lutandika, Mwalimu Omari (Huru), Dafa Francis (Unga Limited), Philemon Mwandesile (Polisi Dodoma), Semi Kessi (Polisi Morogoro), Mustapha Mohamed (Villa Squad) na Bantu Admin (Polisi Dodoma).
.