Dullonet Tanzania | Just Call it Real Solutions for News and Informations
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
Joseph ambaye aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi uliopita, atapata kitita dola za Kimarekani, 200,000 sawa na Shilingi milioni 260 kwa mwaka kwa mujibu wa wakala wa Fifa , Mehd Rehmtullah.

Rhemtullah alisema kuwa huo ni maktaba mnono sana kwa mchezaji huyo ambaye pia utaiwezesha klabu yake kufaidika.

“Haya ni mafanikio makubwa sana kwake, soka la Tanzania na klabu yake, ni mktaba mkubwa ingawa mmchezaji anakabiliwa na changamoto Kubwa ili kuiwezesha klabu hiyo kupata daraja la juu,” alisema Rhemtullah.

Nahodha huyo wa zamani wa Stars alianza kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa miaka kadhaa iliyopita bila mafanikio na sasa ndoto yake imetimia baada ya mkataba huu mnono.

Kwanza alifanya majaribio na timu ya ligi kuu ya Norway, Molde FC na akaumia wakati akiwa kwenye zoezi hilo.

Baada ya kuumia, Joseph alirejea nyumbani na kujiunga na timu yake vile vile Taifa Stars na kuiwezesha timu hiyo kufanya vyema katika mashindano ya CHAN.

Rhemtullah alisema Emeh Izechukwu hajafanikiwa kusaini mkataba wowote kutokana na umri wake kuwa mdogo na kwa mujibu wa sheria, mkataba huo kwa sasa utafanyika Julai 17 mwakani.

Alisema kuwa umri mdogo ulionyeshwa kwenye pasi ya mchezaji huyo ndiyo kikwazo kikubwa na kushindwa kukamilisha ofa hiyo. Mchezaji huyo kwa sasa ana umri wa miaka 17.





















..
.