Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
MABINGWA wa Ligi Kuu Kenya, Mathare United imeanza kampeni za kuwania Kombe la Kagame, vizuri baada ya kuifunga Kartileh ya Djibouti mabao 3-0, katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Merreikh, Khartoum Sudan juzi.
Mabingwa hao wa Kenya walianza mchezo taratibu na kumiliki mpira ambapo mara kadhaa kocha wa timu hiyo, Francis Kimanzi alikuwa akiwapigia kelele.
Said Moussa, kiongozi wa ufundi wa Kartile alikuwa na furaha kwa kipigo hicho, ni mara ya kwanza kuwa nje ya nchi yake, pamoja na kufungwa mabao mengi. "Tutacheza vizuri katika mechi nyingine zijazo," alisema.
Posted by Dullonet: 02.07.2009 Source:
Written by: KHARTOUM, Sudan
Mathare ilikosa mabao mengi kabla ya Chrispin Ochieng, kuifungia bao la kwanza timu yake dakika ya 42, kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Titus Mulama. Jaffer Gichuki aliifungia bao la pili kwa shuti kali, lililopita katika miguu ya kipa, Abdulrahim Youssuf dakika ya 57.
Bao la tatu la Mathare United, inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars', Kimanzi walijipatia bao la tatu dakika ya 75, lililowekwa kimiani kwa kichwa na Anthony Kimani.
Katika mechi nyingine, El Merreikh ya Sudan ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, walianza vyema baada ya kulinda heshima ya nyumbani kwa kuigagadua Atraco ya Rwanda mabao 6-1.