Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
Happybirthday B12, Picha kwa hisani ya Michuzi JR Blog
WAETHIOPIA 31 kati ya 151 walioko mahabusu gereza kuu la Mkoa wa Arusha wamelazwa katika hospitali ya Mount Meru, baada ya afya zao kudhoofu kutokana na mgomo wa kula chakula.
Waethiopia hao walikamatwa na polisi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, baada ya kuingia nchini bila kibali wiki moja iliyopita na hivi sasa wanasubiri taratibu za kisheria za kuwarejesha kwao.
Baadhi yao wamelazwa katika zahanati ya gereza la Kisongo ambao hali zao si mbaya.
Wauguzi hospitalini hapo walisema kuwa pamoja na kupewa maziwa na uji wameendelea kugoma kula.
Posted by Dullonet: 02.07.2009 Source:
Written by: Richard Mwangulube, Arusha
Kwa mujibu wa wauguzi hao, afya za Waethiopia hao zinaendelea kudhoofu kutokana na kugoma kula.
Walieleza kuwa Waethiopia hao wamelazwa
katika wodi chini ya ulinzi mkali wa askari magereza.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, anatarajia kuwasili mkoani Arusha kuwatembelea Waethiopia hao.