Dullonet Tanzania | Wazee wa Yanga wajiweka kwa vita ya Al Ahly.
Home                   Burudani               Chatroom            Contact Us             About Us                       Maintenance
Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
WAKATI kukiwa na taarifa kuwa mchezaji wa Yanga Nurdin Bakari anataka kuvunja mkataba na klabu hiyo na kuhamia Azam FC, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtaka mchezaji huyo atulie mpaka kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Nurdin alionekana takribani wiki mbili sasa akirandaranda kwenye viunga vya TFF ina nadaiwa anasaka mwongozo ili aweze kuvunja mkataba huo.

Mchezaji huyo ambaye ana mkataba wa miaka mitatu na Yanga alikuwa na azma ya kujiunga na Azam kwa muda mrefu na aliwahi kuonywa na kocha wake, Dusan Kondic kuwa asikimbilie Azam kwa kuwa atamsaidia kusaka timu nje ya nchi.
















.


Posted by Dullonet: 01.07.2009
Source:   Mwandishi Maalum
Online Radio Live
Lakini jana TFF iliiambia Mwananchi kuwa mchezaji huyo amechelewa kutimiza azma yake kama kweli alikuwa na nia ya kwenda Azam kwa kuwa hivi sasa kanuni haimruhusu kuvunja mkataba na badala yake asubiri dirisha dogo kama kweli ana nia ya kufanya hivyo.


Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Ufundi Sunday Kayuni alisema, "Nurdin ana mkataba Yanga wa miaka mitatu, tulitoa siku 15 kwa klabu na wachezaji kuacha wachezaji ama kuvunja kwa mikataba siku hile ndiyo mambo yote hayo yangefanyika, lakini hawakufanya hivyo.


" Kisheria, Nurdin haruhusiwi kufanya mazungumzo na klabu nyingine wakati ana mkataba inatakiwa mazungumzo yafanywe na klabu kwa klabu. Pia, kama ni kuvunja mkataba alitakiwa avunje kipindi kilichowekwa na ikigundulika kuwa anavunja mkataba kwa ajili ya ushawishi wa klabu nyingine anachukuliwa hatua na klabu inayomshawishi pia inachukuliwa hatua,"alifafanua Kayuni.


"Lakini mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kama mkataba wake umebakiza miezi sita kumalizika na anaruhusiwa pia kusaini mkataba kwenye klabu nyingine huku akiichezea timu yake ya zamani mpaka mkataba umalizike....,"alisema.


Lakini, Nurdin mwenyewe aliiambia Mwananchi kuwa anafuatilia bima yake TFF, kitendo ambacho kilionyesha kumshangaza Kayuni alipoulizwa kuhusiana na suala hilo.


Kwa upande wake, kocha wake (Kondic) aliwahi kukaririwa akimtaka mchezaji huy kuchagua kubakia au la.
















.


Mchezaji wa kiungo wa Yanga Nurdin Bakari.