Copyright @ 2007 Dullonet.com. All Right Reserved
WACHEZAJI Nizar Khalfani na Nadir Haroub ‘Canavaro’ wataanza mtihani wao wa kwanza kwa timu ya soka ya Vancouver ya Canada Julai 9.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa safari ya wachezaji hao Rahim Kagezi alisema wachezaji hao wanatarajiwa kwenda Canada muda wowote kuanzia sasa.
Wachezaji hao wataenda Canada kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika timu ya Vancouver ambapo mechi yao ya kwanza ya majaribio itakuwa Julai 9.
.
Posted by Dullonet: 01.07.2009 Source:
Written by: Mwandishi Wetu
“Kuna mechi Vancouver itachezwa Julai 9 na katika mechi hiyo Canavaro na Nizar wanatakiwa kuicheza hivyo muda wowote wataondoka,” alisema.
Alisema mbali na Nizar na Canavaro, wachezaji wengine wawili watajiunga na wenzao mara uongozi wa Vancouver utakapokuwa tayari kulingana ratiba yao.
“Mchezaji mwingine atakayekwenda Vancouver na kina Nizar ni Zahoro Pazi, lakini yeye ataondoka wiki mbili zijazo kutoka sasa,” alisema.
Aidha, alisema mchezaji Abdulazaki Khalfani anatarajiwa kuungana Canada na wenzake baada ya mwezi mmoja, lakini yeye atakwenda kufanya majaribio kwenye timu ya Miami.
Timu ya Vancouver ilikuja nchini mwanzoni mwa mwaka huu na kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba, Yanga na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars.
.
Mmoja wa wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kwa majaribio katika klabu ya Vancouver ya Canada Nizar Halfan (kulia) akiwa katika moja ya purukushani katika timu ya Taifa.